Tuesday 17 May 2022

THE NEW KENYAN SPOKEN WORD - DREAMS KWA NATION BY JAY B KIBADY

 Dreams kwa Nation


Niko kwa bed ndogo ya 6 by 4 
Na dreams kubwa za one day sitaomba msee wa boda lift ntakuja kumiliki 4 by 4
Hizi ni dreams nimekua nazo since before 
That hiii country itaamka from its dream na hio day itakua before wanifunike ndani ya 6 by 4 

Dream big kuliko za Martin Luther 
That hatuta important mitumba tuki export leather 
That one day itafika siku ya election na after kura hiii country itakua calm ka weather 
Country ya lugha mob tuishi together 
Hatutakua tunaletwa pamoja December na families gather 
That one day tutakua na wakimbizi less alafu wengi wetu watakua wana riadha

Job zitakua mob so hakutakua na wasee wakujaza hizo rally za wana siasa 
Na mtu akikam kutugawanya na politics tutamwambia wee wacha siasa
Street hazitakua na watoto waku randa randa coz tutakua tumewapiga msasa 
Hii nation tutaipeleka father,,, juuu kwa all nation kwangu Kenya ndio masa 
And that's why nikiwa kwa my country always na feel niko feet kama ile jibu ya "sasa'

Dreams za one day utalala na your door open 
one day utapanda kwa mat na utumie your phone windows zikiwa open 
Not ati juu hakuna mtu atakua ana ku owe peni 
Ni vile tutakua tume close hizo windows za wizi kwa kuweka more job oportunities open 
So mtakua 24 seven mnatembea na shoes za open 
Hata ikifika usiku ile midaa ya ten 
Hautakua unaogopa kutolewa nduki na karao alafu unawacha sleepers kwa barabara juu ya fear na pain 



Dream za day moja sugar company zitatuletea result tamu sio kutupea pressure na Kisukari 
Country ina recycle chuma haita import tena misumari 
Bahati ya Youth haitapatikana tu kwa Kamari 
Ama ati akipata mama/baba ako na madoo ndio am marry
Kwa balot box pesa hazitatutafanya tupige kura in a hurry 
Hizi ni dreams niko nazo na hiii country 


Dream za one day tutaenda shule juu tunataka ku learn 
Not vile tunaenda shule ndio baadae kwa life tu earn 
Nikikusaidia leo kesho hauta ni geuka ikifika your turn 
So hizi ndio dreams nikilala huwa on zina turn 
Dreams zilianza kitambo niki buy chapo paka sai nime buy my own pan 
Dream za one time Kenya itakua country number one 
Na hizo country zingine tuna zi warn,

No comments:

Post a Comment